Kadi za mwaliko za kidigitali

Kila mgeni, amealikwa kwa heshima.

Tunabuni kadi yako ya mwaliko, tunamtumia kila mgeni kadi yake kwa WhatsApp na SMS, tunakusanya majibu yao, na siku ya tukio tunawapokea getini kwa QR-Code.

Harusi · Send-off · Kitchen party · Birthday · Mahafali · Matukio ya kampuni

Ubungo, Dar es Salaam · Tunahudumia Tanzania nzima

Tunachofanya

Mialiko, majibu na geti, vyote mahali pamoja

Kuanzia muundo wa kadi hadi mgeni wa mwisho kuingia, JAXDIGITALS inashughulikia orodha yako ya wageni ili familia yako ifurahie siku yenu.

Ubunifu wa kadi

Kadi maridadi ya harusi, send-off, kitchen party, birthday au tukio la kampuni, kwa Kiswahili au Kiingereza, yenye picha na rangi zako.

Kadi binafsi kwa kila mgeni

Kila kadi ina jina na cheo cha mgeni, aina ya kadi (SINGLE au DOUBLE), namba ya kadi na QR-Code yake.

Kwa WhatsApp na SMS

Kila mgeni anapokea kadi yake kwa WhatsApp, yenye vitufe viwili vya kujibu, na kwa SMS pia. Hakuna anayeachwa.

Majibu, ukumbusho na shukrani

Mnaona nani anakuja kadri majibu yanavyoingia. Tunawakumbusha wageni kabla ya siku, na baadaye tunatuma shukrani pamoja na link ya picha za tukio.

Michango bila usumbufu

Ahadi, malipo na baki kwenye orodha moja. Mweka hazina anaweka malipo, na kila mchangiaji anapata ukumbusho wenye kiasi chake.

QR-Code getini

Kila kadi inascaniwa kwa simu na inaingiza idadi sahihi ya watu, mara moja tu, huku kamati ikiona waliofika moja kwa moja.

Jinsi inavyofanya kazi

Hatua nne rahisi

  1. Tuambie kuhusu tukio lako

    Tutumie tarehe, ukumbi na orodha ya wageni. Excel au orodha ya majina na namba za simu inatosha.

  2. Idhinisha kadi yako

    Tunabuni kadi yenye majina, picha na rangi zako, na tunairekebisha hadi uridhike.

  3. Tunatuma mialiko

    Kila mgeni anapokea kadi yake kwa WhatsApp na SMS, nanyi mnaona majibu yakiingia.

  4. Karibisha wageni siku ya tukio

    QR-Code zinascaniwa getini, na kamati inaona waliofika moja kwa moja.

Bei

Chagua kifurushi cha tukio lako

Bei ni kwa kila kadi ya mwaliko. Kadi ya DOUBLE (watu 2) ni kadi moja.

Basic

Kila unachohitaji kualika kwa hadhi.

TSh 1,500 kwa kadi

  • Kadi ya kidigitali yenye jina la mgeni na QR-Code yake
  • Inatumwa kwa kila mgeni kwa WhatsApp na SMS
  • Wageni wanajibu papo hapo: Nitahudhuria / Sitaweza
  • Ukurasa wa kamati: waliothibitisha na waliofika
  • Ramani ya Ukumbi au Eneo la tukio
  • Mtu wa kuscan getini: bure kuanzia kadi 200. Chini ya hapo TSh 35,000, au tunakupa app ya kuscan na kukufundisha.

Premium

Huduma kamili, kuanzia tarehe hadi michango.

TSh 2,500 kwa kadi

  • Kila kilichopo Standard
  • Ujumbe wa Save the Date, au wa kukumbusha siku moja kabla ya tukio
  • Jumbe za mwisho za kukumbusha michango bure: hadi mara 2 ya idadi ya kadi, kwa WhatsApp na SMS

Huduma inayojitegemea

Michango

Anza kukusanya michango hata miezi kabla ya tukio, kabla ya kadi.

  • Orodha ya wachangiaji: ahadi, kilicholipwa na kiasi kilichobaki
  • Link maalum ya mweka hazina kuweka malipo
  • Awamu 3 za jumbe za kukumbusha michango (WhatsApp na SMS), ambao hawajatoa ahadi, waliotoa ahadi na kiwango na alichokwisha changia
  • Aliyemaliza kulipa hapokei ujumbe tena

TSh 700 kwa mchangiaji

  • Hadi wachangiaji 200, watatumiwa ujumbe awamu tatu
  • TSh 500 kwa kila mchangiaji zaidi ya 200
  • Awamu ya ziada (kuanzia awamu ya 4, 5 na kuendelea): TSh 200 kwa mtu
Uliza kuhusu tukio lako Tuambie tarehe na idadi ya wageni, tutakujibu na bei.

Kuhusu sisi

Kuhusu JAXDIGITALS

JAXDIGITALS ni huduma ya kadi za mwaliko za kidigitali ya Olam Technologies, biashara iliyosajiliwa Tanzania. Tunasaidia familia na taasisi kuwaalika wageni wao kwa njia ya kisasa na binafsi, na kuendesha mlango salama na tulivu siku ya tukio.

Jina la biashara lililosajiliwa: OLAM TECHNOLOGIES
Namba ya usajili BRELA 585622, tarehe 30 Septemba 2024, chini ya Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara

Tuko Ubungo, Dar es Salaam, na tunahudumia matukio Tanzania nzima.

  • Tunatuma ujumbe kwa namba alizotupa mwenye tukio tu, na kuhusu tukio hilo tu.
  • Kila ujumbe unaonyesha nani anakualika na kwa nini.
  • Mgeni anaweza kukataa kwa kubonyeza mara moja, au kutuomba tuache kumtumia ujumbe wakati wowote.
  • Hatuuzi wala kutoa taarifa za wageni kwa matangazo. Soma sera yetu ya faragha.

Wasiliana nasi

Una tukio? Tuongee.

Tuambie tarehe na takriban idadi ya wageni, tutakutumia bei.

WhatsApp
+255 627 404 843
Ofisi
Ubungo, Dar es Salaam
Tunahudumia Tanzania nzima